WAMEFUNGUA MILANGO YOTE YA NCHI NA MADIRISHA PIA!

Waziri wa maliasili na utalii Mh.Kagasheki anaonyesha jitihada zake kama kiongozi wa wizara inayomhusu kwa manufaa ya Taifa. Wakati anafichua madudu yanayofanywa katika wizara; ndani ya mwezi huu wa Agosti, 2012 gazeti la The Guardian lilichapisha matokeo ya utafiti kuhusu sekta ya utalii; utafiti uliofanywa na Makamu mkuu wa chuo kikuu cha St.Augustine Dk.Charles Kitima.

Kwa hakika, matokeo ya utafiti wake yanafikirisha na kuhuzunisha kwa yoyote anayeipenda  nchi hii. Kwa mujibu wa utafiti huo, karibu trillioni 1.2 fedha za Kitanzania zinazopatikana kila mwaka kutoka katika sekta hiyo huishia nje ya nchi (capital flight) yanakotoka mashirika makubwa ya kimataifa multinational companies (MNCs) yanayomiliki hisa nyingi katika biashara ya sekta ya utalii hapa nchini.

Kwa mfano, vitalu vya uwindaji 95% vinamilikiwa na wageni na 05% wakiambulia wazawa. Hii ni sababu kubwa ya fedha nyingi kwenda nje ya nchi. Ingawa utafiti wa Dk.Kitima uligusa sekta ya utalii pekee, ni imani yangu kwamba hali ni hiyo hiyo katika sekta nyingine kuanzia madini, fedha (mabenki), hadi mawasiliano(hasa simu za mikononi/viganjani). Hali hii inatufanya baadhi yetu tuanze kujiuliza kama kweli hii ndiyo stahiki yetu kutokana na kiwewe chetu kipya cha kushupalia wawekezaji wa kigeni!

Binafsi, ninakubaliana na msimamo wa Robert Mugabe(rais wa Zimbabwe); ambaye yeye alishinikiza uwepo wa sheria inayowalazimisha wawekezaji wageni kuwa na ubia na wazawa. Kupitia tangazo la serikali Na.280 la mwaka 2012, ambapo kila biashara kubwa nchini humo 49% humilikiwa na wageni tu na 51% inamilikiwa na wazawa. Na hiyo ni kwa sekta zote za madini, utalii, nishati, usafiri, mawasiliano, elimu, na fedha.

Ingawa Mr. Mugabe alishutumiwa sana kwa uamuzi huo uliotafsiriwa kuwa ni wa kidikteta;lakini ukweli ni kwamba alilenga kuinufaisha nchi yake. Kuwa fanya wazawa wamiliki 51% ya hisa katika kila biashara kubwa, kunahakikisha kuwa angalau mapato ya asilimia hiyo hiyo yanabaki nchini Zimbabwe kila mwaka.

Ikumbukwe kwamba wawekezaji wote wa kigeni wanapoingia katika nchi yoyote huwa hawana lengo lolote la dhati la kuiendeleza nchi husika. Lengo lao kubwa  pekee ni kujitengenezea fedha na kuzipeleka kwao kila mwaka; na ndiyo maana hujiondokea haraka kwa kufunga au kuuza biashara zao wanapoona hawapati tena faida au kipindi cha unafuu wa kodi (tax holiday) walichopewa kimemalizika.

Ndugu zangu, naomba niseme kuwa matokeo ya utafiti wa Dk.Kitima yanafikirisha. Kwangu mimi nayachukulia kama ni kengele ya uamsho kwa watawala wetu ambao wameifanya nchi yetu kuwa shamba la bibi kwelikweli. Ili tu wasifiwe na asasi za Bretton Woods(World Bank na IMF) kuwa wameboresha mazingira ya uwekezaji wa kigeni katika nchi zao! Swali la kujiuliza, mbona wazawa ambao ni ndugu zao wana wanyanyapaa?!

Advertisements

3 Comments

  1. Hivi jamani,hatuwezi kuwatafuta waganga ili watusaidie katika matatizo ya hawa tuliowakabidhi madaraka?Au kama vipi tutafute kundi kama la Alqaida liwateka na kuwapatia mateso makali ili waweze kuwatumikia wananchi vizuri.

    Like

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s