KWA MPANGO HUU UMASKINI LAZIMA

SHERIA YA MADINI NA UWEKEZAJI

Katika sekta ya madini hapa nchini Tanzania wanaonufaika zaidi ni wawekezaji tu na nchi inaambulia kiduchu.

Iko hivi,kwenye kila Tshs 100/= serikali inapata Tshs 3/= na mwekezaji anapata Tshs 97/=.Hicho kiasi serikali inachopata kinaitwa mrahaba;kuhusu kodi wamesamehewa(Tax holiday) kwa madai kwamba walisema wanapata hasara na pia wanafidia gharama za kuwekeza.

Unaweza kujiuliza hasara gani wakati eneo analochimba limekwisha thibitishwa kuwa lina madini na muda wa madini hayo kuisha hapo ardhini umekwisha julikana.

Ila serikali ili kuja kushituka na kuamua kufanya uchunguzi kama kweli tuhuma za wawekezaji katika sekta ya madini ni sahihi,kampuni iitwayo Stewart kutoka Marekani ikapewa kazi hiyo.

Jibu kwa ufupi likawa,serikali inaibiwa kiasi cha robo ya bajeti yake kwa mwaka inayopotelea kwa kuwakubalia wawekezaji kuwa wanapata hasara.

MFANO HAI KATIKA SEKTA NYINGINE

Uwanja wa ndege wa kamataifa wa Kilimanjaro,umebinafsisha kwa mwekezaji mmoja;ambaye anailipa serikali kodi ya dola za kimarekani 1000 kwa mwezi.Na mwekezaji huyo analipwa na shirika moja tu la ndege kama KLM dola za kimarekani 5000 kwa mwezi.

Unaweza kujiuliza tu swali rahisi,je kuna mashirika mangapi ambayo ndege zake zinatua Kilimanjaro International Airport(KIA)?Mimi naamini ni mengi,lakini serikali imekubali kudhulumiwa huku nikiamini wanalijua hilo.Kwasababu,mbunge(Zitto Kabwe) aliomba mkataba huo upelekwe bungeni;cha ajabu waziri mwenye dhamana husika(Zakia Meghji)akamjibu mbunge,haitawezakana kwa madai kwamba mkataba ni siri.

Lakini ukweli uliopo kwa mujibu wa sheria mkataba unaohusu mali ya umma siyo siri

Jingine ni hoteli iliyojengwa hapo awali ikiitwa Sheraton,walipewa msamaha wa kodi wa miaka mitano,baada ya hapo ikaitwa Royal Palm na hawa pia;hadi sasa Movenpick msamaha pia unaendelea kuwepo,baada ya hapo sijui itaitwaje?Yote hii ni kutokana na sera na sheria mbovu za uwekezaji ambapo serikali inachezewa mchezo mchafu na wawekezaji.

Hiyo ni baadhi ya mifano tu,lakini naamini kuna mikataba mingi tu ambayo ipo kwa manufaa ya wageni na nchi zao,huku tukibaki kudai kodi kwenye magenge na maduka bila hata aibu;lakini wale wanaopata mabilioni ya shilingi kwa mwezi hawasumbuliwi kama si kupewa msamaha wa kodi.

Imefikia hatua ya wawekezaji kutudharau wazawa na kuitishia serikali katika utekelezaji wa mambo yake.

Ninachoamini mimi ni kwamba,huwezi ukategemea fedha ya kodi kutoka katika duka la rejareja ili kuipatia serikali mapato ambayo yatafanya bajeti yetu isiwe tegemezi.Kwa kufanya hivyo ni sawa na kuchota maji kutoka katika kisima kwa lengo la kujaza bahari.

Tusiichukie Tanzania,tuwachukie viongozi wake na umaskini wa nchi hii viongozi ndiyo wakulaumiwa.

Advertisements

5 Comments

  1. Mwanangu unatutia ghadhabu,unajua mimi ni hasira sana na watu kama hawa.Sasa unaona wanavyotufanya machizi/vichaa halafu wao wanaigeuza serikali yetu kama biashara zao.
    Mimi mtu kama huyu akiingia kwenye anga zangu nampa kubwa halafu na mteka naenda kumfanyia upekuzi;kwasababu hanatofauti na mwizi anayekuibia nyumbani kwako.
    Endelee kutujuza ili tupate hasira hata tukikutana mwenyewe abadilishe njia kabla hajaambiwa.

    Like

  2. Excellent post. I used to be checking constantly this weblog and I’m inspired! Extremely useful information particularly the closing part šŸ™‚ I take care of such information much. I was looking for this certain info for a long time. Thanks and best of luck. regards

    Like

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s