KABLA YA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA MPYA KUANZA KAZI YAFUATAYO YALITAKIWA KUJIBIWA KWANZA

A: MFUMO WA SERIKALI
Wananchi walipaswa kuulizwa ni aina gani ya serikali wanayoitaka
(i) serikali moja (ii) serikali mbili (iii) serikali tatu

B:KUHUSU MUUNGANO

(i) uwepo (ii) usiwepo

C: KAMA MUUNGANO UNATAKIWA KUWEPO

Uweje na mambo gani yawe ni ya muungano

Yote haya yangejibiwa na wananchi kwa utaratibu wa kupiga kura ya maoni; baada ya mwongozo huo kuwa tayari basi tume ya kukusanya maoni ingeanza kazi yake.
Hii ingerahisisha kazi/nguvu inayofanywa na watu/vyama vya siasa/taasisi za kijamii kushawishi wengine aina ya serikali inayofaa. Wakati mambo haya yalipaswa kuwa na majibu rasmi kabla hata ya bunge la katiba kuteuliwa na kuanza kazi ya kujadili rasimu ya katiba ilikuja na katiba mpya ya Tanzania.
Naweza kusema kwa kiasi fulani wananchi wamedhulumiwa; na kuacha mambo haya ya msingi kupatiwa majibu na kundi/kikundi fulani cha watu kuwajibia wananchi badala ya wao kupatiwa nafasi ya kutoa majibu yao. Hii ni aibu tunaposema tunataka katiba ya nchi bila ya wananchi kushirikishwa kwenye kila hatua ya msingi inaonyesha ni jinsi gani ubinafsi unavyohusudiwa tena mbaya zaidi katika mambo ya msingi ambayo yana maslahi kwa umma wa watanzania.

Advertisements

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s