HII IMEKAA VIZURI

Sudan ya kusini imekuwa ni nchi ya 54 barani Afrika na ya 193 duniani.Ni baada ya kupata uhuru wake kutoka Sudan ya kaskazini usiku wa kuamkia Jumamosi ya tarehe 09/07/2011.

Na pia,ndiyo nchi ambayo ina mlingoti mfupi wa bendera;ambao unaendeshwa kwa remote control.

Nafikiri kama mnatafuta maendeleo kwa muda mrefu mkiwa pamoja na bado hakuna maendeleo hayo mnayoyatarajia;basi nafikiri ni bora mkajitenga na kuendelea kutafuta kila mmoja kwa juhudi zake.

Nafikiri kwa nchi kama Tanzania ambayo tangu ipate uhuru wake  mwaka 1961 hadi sasa ni kama miaka 50 lakini cha ajabu inashindwa kumudu vitu vya msingi katika maendeleo kama umeme wa uhakika,maji ya kutosha,barabara za uhakika ambazo zinapitika kipindi chote cha mwaka.Hivi kweli inaingia akilini, jijini Dar es salaam maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani,mtu ananunua ndoo Tshs 250-300/=,anakosa umeme kwa muda usiopungua saa6-12 kwa siku!!Yaani kupata uhuru ndiyo kushindwa kujimudu?Na sema hivyo kwasababu;vitu tulivyoachiwa na mkoloni mpaka sasa tunavyo na tunaendelea kujivunia navyo.Vya kwetu baada ya ukoloni kila tukitengeneza havidumu!Unakuta miundoni mbinu ya umeme ipo lakini,nishati yenyewe inapatikana kwa mgao;hata maji pia?!Tena sehemu nyingine hata hiyo miundo mbinu umeng’olewa na kuuzwa kama vyuma chakavu(scrapers) na hiyo yote ni baada ya watu kuona hakuna matumizi yake.

Mijini hali yenyewe ndiyo hiyo;sasa huko vijijini itakuwaje jamani!!Hii ndiyo nchi inayoitwa Tanzania.Nafikiri kuna haja na sisi pia tukachukua uamuzi kama wa Sudan ya kusini,ninasema hivyo kwasababu huenda nchi ni kubwa kiasi kwamba inashindikani au inakuwa ni vigumu kuwapatia watu wake huduma muhimu ambazo ndizo kichocheo cha maendeleo ya mmoja mmoja na hatimaye kwa ujumla wake(taifa).Ninaamini kwa kujitenga,watu wanakuwa na uchungu na rasilimali zao na uzalendo unakuwa ni wa juu zaidi hivyo basi matukio ya ya ufisadi ya kuwa adimu mno pengine hakuna kabisa.

Nawapongezi wananchi wa Sudan ya kusini;na ninaamini wanaweza kupiga hatua za maendeleo haraka zaidi na kuzifikia na hata kuzipita nchi zingine ambazo zimepata uhuru miaka mingi iliyopita.

Advertisements

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s