DHIHAKA NDANI YA BUNGE LA KATIBA

Nadhani ama hadidu za rejea za Bunge hili la Katiba hazikueleweka au hazikutosha kueleweka sawasawa. Hivi vioja vinavyoshuhudiwa, vinaifanya nchi idharaulike kimataifa. Lakini pia, naamini kuwa vinachelewesha kupatikana kwa Katiba mpya au kufikiwa kwa malengo ya uundwaji wa Bunge lenyewe ambalo ndilo lengo kuu. Hivi hakuna Chombo kinachoweza kusimamisha upuuzi huu?

Yaani lolote linaloweza kuokoa Taifa kwenye dhihaka hii kinahitajika kufanyika mapema. Naamini viongozi au Kiongozi aliewateua ana fursa ya Kikatiba kabisa, kuitetea nchi kwa kuepusha uendeaji wa dhihaka zinazoendelea Bungeni sasa.

Tatizo/kosa lilofanyika ni hili hapa

Msishangae kabisa huo ndio ukweli. Ukichunguza mfumo, unaotumika kupata viongozi (wabunge) kwenye vyama utaridhika na hayo majadiliano ndio hadhi yao. Utakuta vyama vinahakikisha anayeshinda ni mtu wanaemmudu internally. Ukiona mtu anasema huyu nammudu ninkwamba kamzidi elimu na uwezo wa kutafakuri mambo. Matokeo yake walio kule maskini ndio hivyo hivyo tuvumilie na tujue hakuna quality product pale labda wananchi wapinge tuanze upya.

Lakini pia, umeshamiri ushabiki wa vyama katika bunge lolote linaloitishwa hapa Tanzania; wakati malengo yanayo wapeleka pale ni ya taifa na si chama. Mijadala inaendeshwa kwa kuegemea vyama badala ya taifa; hii ni aibu kwa taifa mbele ya mataifa mengine yanayofatilia mambo yanavyoendeshwa hapa nchini.

Kilichotakiwa kufanyika ili kuepukana na aibu inayoendelea hadi hivi sasa

Ni kweli kabisa tuendelea kuaibishwa na mabunge yote yanakaa kujadili mambo ya nchi/Tanzania ,ilitakiwa wajumbe wengi wawe ni watu wasiyo wanasiasa wa kutoka katika vyama.Bali wawe ni kutoka makundi ya kijamii na wanasiasa wachanyike kwa kiasi kidogo sana/wachache tu.Hapo ndipo tungeepukana na aibu hii tunayoipata na huenda tukaendelea kuipata dhidi ya mataifa mengine duniani yanayoitazama Tanzania.

 

 

Advertisements

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s