DENI LA TAIFA LINATISHA

Naibu Waziri wa fedha amesema,hadi hivi sasa deni la Taifa limefikia dola za Marekanikani 15.9 billioni ambazo ni sawa na Tshs.trillioni 22;pamoja na ukubwa wa deni hilo naibu waziri amesema Tanzania bado inakopesheka.Aliongeza kwa kusema, kutokana na raslimali nyingi tulizonazo(Tanzania);zinawezwa kuwekwa rehani na nchi ikajipatia fedha kwa njia ya mkopo.
Wakati huohuo rais amekwisha tangaza matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika August,2012; matakeo yameonyesha kuwa hivi sasa Tanzania ina watu 44,900,000 idadi ambayo imemshitua rais na kukusisitiza uzazi wa mpango uzingatiwe.Pia, makarani wa sensa hadi hivi sasa wadai serikali(wizara ya fedha) malimbikizo ya posho zao; ambapo inaonyesha kila mtu alikuwa analipwa siyo chini ya Tshs 450,000/= kwa jumla.
Katika deni hilo la makarani wa sensa,waziri fedha amekiri na kuahidi kutatua tatizo hilo haraka.Hii ni alipokuwa kuwa anamjibu rais kuhusu madai hayo.
Wakati huo huo, deni la Taifa linanishangaza kuna taarifa zinasema hivi sasa ni Tshs trillioni 22{Naibu waziri wizara ya fedha} na nyingi ni Tshs billioni 620{Gazeti la Mwananchi};
Deni la walimu pekee yake kwa serikali ni Tshs billioni 25.
Vile vile serikali inasema makampuni ya simu yanalipa kodi nyingi;hapa unaweza kujiuliza kodi yenyewe ni ipi?Kama ni VAT{Value Added Tax=kodi ya ongezeko la thamani} hii inalipwa na watumiaji/walaji na siyo kampuni; hapa ina maanisha kampuni zinasimama kama wakala wa serikali katika kukusanya, swali hapa linabaki kampuni zinalipa kodi ipi hapa nchini Tanzania? Kwa kawaida hakuna ukomo katika kukusanya raslimali/mapato ila kuna ukomo katika kutumia ulichokusanya tofauti na hivyo kuna walakini. Hapa inaonyesha kuwa serikali imeridhika na mapato wanayopata, au ubunifu =0. Wakati huohuo watanzania wakiendelea kusumbuliwa na umaskini, huku huduma zinazotelewa zikiwa ni duni na hazi watosheleze watanzania wote. Lakini pia, serikali haina nia ya dhati katika zoezi la kupambana na kubana matumizi ya fedha zinazopatikana; kwa kuepuka shughuli au masuala yasiyokuwa ya msingi; mfano kununua magari ya gharama kubwa, kuingia katika mikataba isiyokuwa na maslahi kwa umma/Taifa, posho za vikao na safari zisizokuwa na maslahi/tija kwa Taifa iwe ndani au nje ya nchi.

Advertisements

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s