CHADEMA NA TEKNOLOJIA KAZINI

CHADEMA ilitumia mitambo maalum ya
DVR kurekodi mkutano wa
tarehe 15/06/2013
Imethibitika kwamba technology ya mawasiliano hivi sasa
imekua kwa kasi ya ajabu sana, kiasi chakufikia kuwa
kumbe siyo lazima tutegemee camera za waandishi wa
habari kuchukua matukio.
Ni kwamba chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA kwenye mkutano wake wa mwisho licha ya
kutumia setlite kurekodi mikutano yake, imethibitika kuwa
chama hicho kilitumia mtambo maalum wa mawasiliano
kurekodi mkutano wake wa mwisho katika uwanja wa
soweto Arusha. Mtambo huo ambao unauwezo wa
kurekodi matukio kwa masaa 72 mfululizo bila kuhitaji
chaji, ulifungwa sehemu maalum ili kuweza kunasa matukio
yaliyokuwa yanaendelea kwenye mkutano.
Mtambo huo ulisaidia kunasa tukio la mlipuko wa bomu na
matumizi ya risasi kwenye mkutano kuwapiga raia,
ambapo ulionyesha askari polisi aliyesimama pembeni ya
nguzo yaumeme karibu na mfereji ulio mkabala na round
about iliyo karibu na soweto garden akiwapiga risasi watu
waliokuwa wanamkimbiza mtu aliyevaa suruali ya jeans
aliyekimbia nakuingia kwenye gari ya polisi na kuondoka kwa
kasi kwenye eneo la tukio. Mtambo pia uliwezakuonyesha
gari ya blue landcruiser iliyoweza kui escort gari ambayo
amepanda tule mtu aliyekuwa anakimbizwa.
Ule mtambo ambao una uwezo wa kurekodi matukio kwa
around360 degree angle uliweza kuonyesha tukio la watu
wanaosadikiwa kuwa maaskari kufika kwenye eneo la tukio
hasa kwenye gari la matangazo la chadema majira ya usiku,
na kuweza kuzurura pale bila kuonyesha kwa kina
walichokuwa wanakifanya pale.
video inaonyesha ule mtambo ulizima wenyewe saa moja
na madakika asubuhi ya siku ya pili.
Kwa ujumla mtambo una taarifa nyeti za kuweza kusaidia
kwa ushahidi wa tukio hili ambalo limegharimu maisha wa
watu wasiokuwa na hatia. Muda utakapofika nadhani kwa
idhini ya mwenyekiti wa chama kila kitu kitawekwa wazi.

Advertisements

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s