MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KUBAKIA MIWILI TU IFIKAPO MACHI, 2018.

Ukomo wa mifuko mitano ni Machi, 2018 na mifuko miwili kuimarishwa au kudumishwa ambapo idadi ya wanachama, madeni, kesi au madudu yeyote kutoka mifuko mitatu hiyo kukabidhiwa, kurithiwa na kuridhiwa na mifuko miwili ambayo ni PSPF na NSSF. Kwani Tarehe 6 Novemba 2017 mifuko hiyo mitatu imepewa amri ya kupeleka idadi ya wanachama, mali zote, madeni na kesi zote kwaajili ya utayari wa kumilikiwa.

Sasa utitiri wa mifuko Tanzania Bara sasa unafikia kikomo ambapo SSRA atapumua na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuanzia mwezi Machi 2018 kutoka mifuko mitano (PSPF, NSSF, PPF, LAPF na GEPF) kufikia miwili; awamu ya tano imefanya maamuzi magumu na yenye busara kabisa.

Awamu ya nne ya Jakaya ilikuwa na huo mpango wa kuunganisha mifuko lakini zoezi lilikuwa linasusua.

Kuna sekta mbili ambapo mifuko miwili itaimarishwa na mitatu kumezwa. Mfuko wa PSPF utachukua wanachama wote wa public sector kutoka mifuko ya PPF, GEPF na LAPF.

Mfuko wa NSSF utachukua wanachama wote wa private sector kutoka PPF, GEPF na LAPF.

Wakati NHIF itaendelea kusajili wanachama kutoka public na private sector pasipo kikwazo cha umri na utaendelea kutoa huduma ya kiafya kwa mwanachama wake mpaka ukomo wa maisha yake.

Angalia mchakato kwa chati.

upload_2017-11-21_11-16-25.png

Advertisements

NI MFANO MZURI

Tusiilaumu Tanzania bali tuwalaumu viongozi wake; haiwezekani kwa nchi tajiri kama Tanzania kwa muda wa miaka 56 tangu tumepata uhuru bado tuna bajeti tegemezi, barabara mbovu, hatuna maji ya uhakika, umeme wa mgawo,…….(mijini & vijijini). Halafu ni nchi ya amani na utulivu lakini bado tumeshindwa kufanikiwa hadi leo hii!
Lazima kuna tatizo katika mfumo na bechi la ufundi limeshindwa kutatua dosari za mfumo unaotumika ili kuleta matokeo mazuri=ushindi; unajua hata unapokuwa kwenye mchezo hasa ule unaopendwa na wengi duniani (football) ukiona timu yako kadri muda unavyoenda hakuna matokeo mazuri kocha akishirikia na bechi la ufundi anatakiwa afanye yafuatayo 1. kubadilisha formation ya mchezo 2. kufanya substitution ya baadhi ya wachezaji (mipango ya wakati huo); endapo wamiliki wa timu bado wana imani na kocha wao anaweza kuendelea na hatua ifuatayo katika kujiimarisha 3. kusajili wachezaji wapya na kuondoa baadhi yao kama kuna ulazima wa kufanya hivyo (mipango ya baadaye).
Lakini pia, kocha anaweza kujiuzulu au kufukuzwa na wenye timu.
Kwa kutumia mfano huo, matokeo mazuri kwa Tanzania 1. kuwa na bajeti inayojitosheleza bila mikopo wala misaada kutoka kwa nchi wahisani 2. kuwa donor country-kuzisaidia nchi nyingine kifedha (msaada au mikopo). Kwa miaka 56 tangu uhuru hatujashinda japo kikombe kimoja wapo tu kati ya hivyo viwili?! Maamuzi magumu yanatakiwa ili kuinusuru timu.
Je, ni kweli wenye timu wameridhika na mwenendo wa timu inavyoendeshwa?

Tetesi: Tanzania yadaiwa kujiondoa kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji(OGP)

Serikali ya Tanzania inadaiwa kujitoa kwa muda kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji yaani Open Goverment Partnership(OGP). Inadaiwa Serikali imeamua kujikita kwenye “kutumbua majipu” kwanza kabla ya kujikita kwenye uwazi.

OGP ilianzishwa mwaka 2011 na ilianza na Serikali 8 hadi 70 na Tanzania ilijiunga 2011 na kutekeleza mipango kazi ya kitaifa mitatu hadi sasa (3 National Action Plans).

Ahadi 7 zilizokuwa kwenye Mpango Kazi wa tatu wa Kitaifa wa OGP ni

i) Kutungwa kwa Sheria ya Upatikanaji wa Habari(Access to Information Act)

ii) Bajeti kuwa wazi(Open Budgets)

iii) Taarifa mbalimbali za Serikali kuwa wazi(Open Data)

iv) Uwazi wa masuala ya ardhi ikiwemo taarifa za umiliki wa Ardhi nchi nzima kuweza kupatikana mtandaoni(Land Transparency)

v) Uwazi katika Sekta ya Madini

Ahadi za Nyongeza
(vi) Uwazi katika Sekta ya Afya kwa ujumla(Medical and Health Service Transparency)

(vii) Kuwepo kwa mifumo ya utendaji kazi wa Serikali iliyo wazi kabisa (Performance Management Systems)

Anaandika Mbunge wa Kigoma Ujiji, Zitto Kabwe:

Nimeshangazwa na uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP. Hivyo nimeamua kuwasilisha swali Bungeni kutaka maelezo ya Serikali, inayojipambanua kwa kupambana dhidi ya ufisadi, kujiondoa kwenye jukwaa la Kimataifa linalopigania Serikali kuendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji.

Uwazi ( Transparency/Openness ) ni silaha muhimu sana katika vita dhidi ya rushwa na katika kuwezesha ufanisi Serikalini.

Licha ya kwamba Tanzania ilikuwa haitimizi ahadi zote kwenye Action Plans, lakini kulikuwa na msingi kwamba Nchi yetu inaamini katika Uwazi na Uwajibikaji. Uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP unarudisha nchi yetu nyuma. Ni uamuzi ambao haukufikiriwa sawa sawa.

Kujua Zaidi kuhusu OGP:

Msafara wa Kikwete Brazil Kwenye Mkutano wa OGP

OGP announces 15 subnational govt that will be part of a pilot program, Kigoma Tanzania one of them

Mpango Kazi wa Kitaifa wa kuendesha shughuli za Serikali kwa Uwazi Awamu ya Tatu (OGP NAP III)

MAGAZETI YOTE NCHINI TANZANIA LAZIMA YASAJILIWE UPYA

Leo Jumatano Agosti 23 saa nne kamili asubuhi Msemaji wa Serikali, Dokta Hassan Abbas amezungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa Habari Maelezo.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, amesema kuwa mfumo mpya wa utoaji wa leseni kwa machapisho yote umeanza rasmi leo Agosti 23,2017. Hivyo basi kuanzia leo hadi Octoba 15 magazeti yote yahakikishe yanakuja kusajiliwa upya.

Pia machapisho ya serikali na taasisi binafsi ni lazima yasajiliwe ambapo taratibu zote za upatikanaji wa leseni zimewekwa katika tovuti ya Home | TANZANIA INFORMATION SERVICES-MAELEZO amesema Dkt. Hassan Abbas.

BIG RESULTS NOW{BRN}

Achana na maneno ya Kilimo kwanza, Maisha Bora kwa kila Mtanzania; ambayo hadi leo sijui kama yameleta mabadiliko chanya kwa watanzania. Tukiwa bado hatuja kaa vizuri na kuona matokeo ya hizo kauli kuu mbili kama tumepiga hatua, tuko pale pale, au tumerudi nyuma.

Hivi sasa tuko kwenye mpango mwingine wa maendeleo ya Taifa unaosema:

Vision 2025/Dira 2025

BIG RESULTS NOW-BRN- (MATOKEO MAKUBWA SASA)

Baadhi ya yanayo tukabili ikiwa ni changamoto kwa  nchi na matokeo halisi bila hata kuumiza kichwa; ni kama ifuatavyo:

Deni la Taifa ni kigugumizi

Uwezekano wa deni la Taifa la Tshs.30 trillioni kuwa ni zaidi ya hilo upo; taarifa ya TCDD na CAG zinathibitisha hilo. Tatizo liko kwenye mikopo inayochukuliwa na serikali fedha zake hazina haiweke kumbukumbu za kuonyesha matumizi ni yapi na kiasi gani kimebakia. Hii inaonyesha matumizi mabaya ya fedha za mikopo; na serikali inapoteza kupitia wizi a.k.a wizi wa kuaminiwa.

Kupunguzwa kwa wafanyakazi kwenye viwanda vya sukari

“Yanayoendelea katika biashara ya sukari nchini ni zaidi ya ESCROW” -Mwenyekiti PAC

Hali halisi iko hivi, mahitaji ya nchi ni tani 420,000 na kiasi kinachozalishwa na viwanda 4 vilivyopo sasa ni tani 320,000. Kwa maana hiyo nchi ina upungufu wa tani 100,000.

Wenye viwanda waliingia makubaliano na serikali itoe vibali vya kuingiza sukari kutoka nje kwa kiasi cha tani 100,000; cha ajabu, sukari inayoingia ni zaidi ya tani hizo walizokubaliana na inauzwa kwa bei nafuu kuliko inayozalishwa hapa nchini. Hii ina maanisha kwamba, serikali imekiuka/imevunja makubaliano na wenye viwanda, na kuna uwezekano mkubwa wa ukwepaji kodi kwa bidhaa hiyo inayotoka nje ya nchi.

Imepelekea biashara kuwa ngumu kwa wazalishaji wa ndani kiasi cha wakulima wa miwa kushindwa kuuza miwa na kulipa madeni yao, viwanda vimelazimika kupunguza wafanyakazi na kuna uwezekano wa kufungwa viwanda.

Ujenzi na muda unaopotezwa kwa safari zinazotumia barabara zetu hapa nchini

Kuna utafiti uliofanywa jijini Dar es salaam; foleni Dar es salaam yazua maradhi mapya utafiti waonyesha tunapoteza Tshs.655 billioni kwa mwaka, kuongeza machizi, kuharibu ndoa.

Mengineyo

Migogoro ya wakulima na wafugaji nchini kote

Balaa la akaunti ya ESCROW Tegeta….n.k

JINSI FURSA ZINAVYOTUMIKA KATIKA TUKIO ZIMA

STORY FUPI YENYE MAFUNZO….
KUNA WIZI UMETOKEA BENKI
•••••••••••••••••••••• Jambazi “wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu”.
Wote wakalala chini.
HII INAITWA DHANA YA USHAWISHI – kubadilisha
njia ya kawaida ya kufikiria.
•••••••••••••••••••••
Kuna dada, kwa woga, akawa amelala chini
kimitego, jambazi akamwambia, “dada hebu kuwa na adabu, chukua kanga jifunike, hili ni tukio la ujambazi na sio la ubakaji.”
HUU UNAITWA WELEDI –
zingatia ulichofundishwa
kufanya.
•••••••••••••••••••••••
Walipotoka kwenye wizi
jambazi mdogo, ambaye
anashahada ya uzamili ya
biashara, akamwambia
mwenzake, “tuzihesabu hizi fedha.” Yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu, “wewe. mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu, saa mbili
watatutangazia kwenye
taarifa ya habari tumeiba
kiasi gani.
HUU INAITWA UJUZI – Siku
hizi ujuzi ndio bora kuliko
vyeti.
••••••••••••••••••••••• Baada ya majambazi kuondoka, meneja akamwambia mhasibu wa bank, “ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi.”
HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI – kushabihiana na mazingira magumu kwa faida binafsi.
•••••••••••••••••••••••
Mhasibu akafurahi na kusema, “dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana.”
HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA – Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi.
••••••••••••••••••••••• Meneja kafurahi sana kwakuwa sasa matatizo yake yametatuliwa na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU – shikilia nafasi pale inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi gani.
•••••••••••••••••••••••
Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki.
Majambazi kuskia hivyo
wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu. Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, “dah! yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli? Bora umeneja kuliko ujambazi.
”HII INAITWA ELIMU NDIYO KILA KITU – ishike sana elimu, ina nguvu kuliko dhahabu.

Je, tunaweza kuhamishia ujanja kama huu kwenye kusaini mikataba ya uwekezaji na nchi ikafaidika kuliko kuwafaidisha wawekezaji?