BIG RESULTS NOW{BRN}

Achana na maneno ya Kilimo kwanza, Maisha Bora kwa kila Mtanzania; ambayo hadi leo sijui kama yameleta mabadiliko chanya kwa watanzania. Tukiwa bado hatuja kaa vizuri na kuona matokeo ya hizo kauli kuu mbili kama tumepiga hatua, tuko pale pale, au tumerudi nyuma.

Hivi sasa tuko kwenye mpango mwingine wa maendeleo ya Taifa unaosema:

Vision 2025/Dira 2025

BIG RESULTS NOW-BRN- (MATOKEO MAKUBWA SASA)

Baadhi ya yanayo tukabili ikiwa ni changamoto kwa  nchi na matokeo halisi bila hata kuumiza kichwa; ni kama ifuatavyo:

Deni la Taifa ni kigugumizi

Uwezekano wa deni la Taifa la Tshs.30 trillioni kuwa ni zaidi ya hilo upo; taarifa ya TCDD na CAG zinathibitisha hilo. Tatizo liko kwenye mikopo inayochukuliwa na serikali fedha zake hazina haiweke kumbukumbu za kuonyesha matumizi ni yapi na kiasi gani kimebakia. Hii inaonyesha matumizi mabaya ya fedha za mikopo; na serikali inapoteza kupitia wizi a.k.a wizi wa kuaminiwa.

Kupunguzwa kwa wafanyakazi kwenye viwanda vya sukari

“Yanayoendelea katika biashara ya sukari nchini ni zaidi ya ESCROW” -Mwenyekiti PAC

Hali halisi iko hivi, mahitaji ya nchi ni tani 420,000 na kiasi kinachozalishwa na viwanda 4 vilivyopo sasa ni tani 320,000. Kwa maana hiyo nchi ina upungufu wa tani 100,000.

Wenye viwanda waliingia makubaliano na serikali itoe vibali vya kuingiza sukari kutoka nje kwa kiasi cha tani 100,000; cha ajabu, sukari inayoingia ni zaidi ya tani hizo walizokubaliana na inauzwa kwa bei nafuu kuliko inayozalishwa hapa nchini. Hii ina maanisha kwamba, serikali imekiuka/imevunja makubaliano na wenye viwanda, na kuna uwezekano mkubwa wa ukwepaji kodi kwa bidhaa hiyo inayotoka nje ya nchi.

Imepelekea biashara kuwa ngumu kwa wazalishaji wa ndani kiasi cha wakulima wa miwa kushindwa kuuza miwa na kulipa madeni yao, viwanda vimelazimika kupunguza wafanyakazi na kuna uwezekano wa kufungwa viwanda.

Ujenzi na muda unaopotezwa kwa safari zinazotumia barabara zetu hapa nchini

Kuna utafiti uliofanywa jijini Dar es salaam; foleni Dar es salaam yazua maradhi mapya utafiti waonyesha tunapoteza Tshs.655 billioni kwa mwaka, kuongeza machizi, kuharibu ndoa.

Mengineyo

Migogoro ya wakulima na wafugaji nchini kote

Balaa la akaunti ya ESCROW Tegeta….n.k

Advertisements