TANESCO BADO IKO KWENYE WASHA HALAFU ZIMA HADI LEO

Hadi hivi sasa ninasikitishwa kwa kiasi kikubwa kwa hili kampuni pekee linalozalisha na kutoa huduma ya umeme nchini Tanzania;hadi hivi sasa sifurahishwi na utendaji wao wa kazi hata kidogo.Nishati ni kichocheo kikubwa cha ukuaji au kudorora kwa uchumi wa nchi yeyote ile hapa katika sayari inayoitwa dunia.

Kwa maana ifuatayo, kunatakiwa kuwe na umeme wa uhakika kwa kipindi chote na kama kuna tokea hitilafu ziwe ni za kiufundi na iwe ni dharula tu na siyo kuwa tatizo la mara kwa mara kila mwaka; lakini pia,umeme unatakiwa uwe unapatikana kwa bei nafuu ili wananchi walio wengi waweze kumudu kuutumia(yaani iwe ni bidhaa ya msingi) na siyo kuwa anasa kwao kuutumia.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na matatizo yale yale ya kila mwaka yaani kuwasha na kuzima umeme kiholela bila kutoa matangazo katika vyombo vya habari ili watu wajiandae; hali inayofanya watu waanze kuamini huenda kuna mgao wa umeme umeanza kimya kimya bila kutangaza kwa kuona aibu.Majibu yaliyotolewa na TANESCO ni kutokana na hitilafu katika chanzo cha kusafirisha gesi, na upungufu wa maji.

Hili la TANESCO kuendelea kutumia na kuutegemea umeme wa nguvu za maji ni tatizo la muda mrefu sana; maji yenyewe yanayotegemewa ni hadi mvua inyeshe vizuri na hii ni aibu; kutumia maji kuzalisha umeme sidhani kama ni tatizo!Ila tatizo ni pale unapoweka mitambo kwenye maji ambayo siyo ya uhakika kwa kipindi cha mwaka mzima hapa ndipo aibu ilipo ili hali kuna mito hapa nchini Tanzania inatiririsha maji mwaka mzima mfano mzuri mto Rufiji lakini pia unaweza angalia uwezekano wa kuzalisha umeme kutoka baharini kama wanavyofanya India na pia kupitia maziwa yaliyoko hapa nchini na bwawa yawe msaada kwa wakulima na wafugaji.Ila cha ajabu TANESCO wakaenda kuweka mitambo kwenye bwawa la Mtera ambalo uhakika wa maji yake ni mvua lakini vilevile kina chake kinaathiriwa na tope kila mara; katika hili waweza sema ni matatizo ya kujitakia tu.

Hali ilivyo sasa tuna kuwa na mitambo mingi ya aina nyingi kwaajili ya kuzalisha umeme lakini hakuna kilichobadilika kwa kiasi cha mtu kujivunia uwekezaji uliofanyika ukilinganisha na kiasi cha fedha kinachotumika kuendesha shughuli za kampuni husika na umeme wenyewe unaopatikana bado hautoshi/haukidhi mahitaji.Na ndiyo maana bado washa-zima iko pale pale hadi hivi sasa

Matumizi ya shirika/kampuni kwa siku yako kama ifuatavyo:

Mitambo inayotumia mafuta ya dizeli zinatumika lita 1,300,000 kwa siku

Mitambo inayotumia mafuta mazito zinatumika lita 500,000 kwa siku

Mitambo inayotumia mafuta mepesi ya ndege(H1) zinatumika lita 500,000 kwa siku

Gharama ya umeme unaozalishwa mitambo ya gesi ukipata utaijumlishia hapo

Na matumizi ya TANESCO katika shughuli zake kwa siku ni billioni 5.4Tshs; wakati makusanyo yake ni billioni 2.34Tshs, kwa maana hiyo kuna upungufu wa billioni 3.06Tshs kwa siku, lakini pia tunaambiwa kuna upungufu wa maji katika vyanzo vya kuzalisha umeme ila haijulikani katika hili la maji mapungufu yake ni kwa siku/wiki/mwezi/miezi/mwaka/miaka?!?

Kwa gharama zote hizo lakini bado tu umeme hautoshelezi mahitaji ya wateja wake ambao ni wachache ukilinganisha na idadi ya Watanzania wanaofikia milioni kama 45.9 ambapo ni 14% ya Watanzania ndiyo wanaotumia umeme nchi nzima.

Advertisements

1 Comment

  1. Yaani hilo shirika ni muhimu kweli;lakini cha ajabu wizara husika haitambui hilo hadi sasa!Hivi kweli kwa kipindi ambacho Tanesco imeanzishwa hadi hivi sasa bado kuna mgao tu.Hapa ndipo unapogundua serikali(wizara) husika haifahamu hata huo umuhimu wa kuwepo kwa shirika hili;hii ina maanisha Tanesco muhimu lakini ndiyo shirika mdebwedo.

    Like

Acha maoni yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s