KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO NCHINI TANZANIA

Kwa yeyote mwenye malalamiko au kero zinazohusiana na huduma za mawasiliano hapa nchini Tanzania; fika/peleka kero au malalamiko yako kwa njia hizi:

1.Baruapepe: info@tcra-ccc.go.tz

2.Fika mwenyewe makao makuu ya NSSF(Nyerere Pension Tower) makutano ya barabara ya Bibititi Mohammed na Morogoro.

Na siyo kulalamika mitaani, ambapo hakutakusaidia zaidi ya kuishia kukasirika tu. Ni vizuri ukatumia njia hizo hapo juu kupeleka yanayokukera/kukukwaza kuhusu huduma za mawasiliano.

Advertisements

Je, serikali yaweza kufanya lolote, vyovyote, kwa yeyote na wakati wowote?

Jibu:

Serikali ni binadamu

Nikama sisi (binadamu) ; hakuna serikali inayoendeshwa kwa mashine au maroboti.

Kwa vile serikali inaongozwa na binadamu basi ina tabia zile zile za kibinadamu. Mfano serikali hudanganya, hukandamiza, hudhulumu, na wakati mwingine serikali au kwa jina la serikali watu wamepoteza uhai (maisha yao).

Serikali hubanwa na katiba na sheria

Kutokana na serikali kuwa na hulka hizo za kibinadamu; jamii mbalimbali ziliamua kujitungia katiba na sheria mbalimbali ili kudhibiti serikali.

Ukweli ulio dhahiri ni kwamba, inaweza kufanya yale tu ambayo inaruhusiwa kufanya ndani ya katiba. Serikali haiwezi na haipaswi kufanya jambo lolote lililo nje ya yale ambayo imepewa kwenye katiba.